DAWASA YAWAITA WAKAZI WA MLALAKUWA HADI MBEZI
15 Sep, 2023
Habari njema kwa wakazi wote wa maeneo ya Goba, Tegeta A, Mbezi Louis, Matosa, Makabe, Mlalakuwa kuwa ofisi za DAWASA MAKONGO inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi.
Zoezi hilo linaenda sambamba na utoaji wa elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano na malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.
Takribani wateja zaidi ya 100 wa maeneo hayo wanatarajia kuanza kunufaika na huduma ya majisafi.
Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0736602601 (DAWASA Makongo)