DAWASA YAWAITA WAKAZI MAKONGO HADI TEGETA 'A' MAUNGANISHO HUDUMA YA MAJI
23 Feb, 2024
Habari njema kwa wakazi wote wa maeneo ya Makabe, Tegeta A, Matosa, Makongo Juu, Mlakakuwa, Goba na Changanyikeni kuwa ofisi za DAWASA Makongo inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi.
Zoezi hilo linaenda sambamba na utoaji wa elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano na malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.
Takribani wateja zaidi ya 200 wa maeneo hayo wanatarajia kunufaika na huduma ya majisafi.
Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au
0736- 602601 (DAWASA Makongo).