Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA YAONGEZA MAWASILIANO NA WATEJA UKONGA - ILALA
23 Feb, 2024
DAWASA YAONGEZA MAWASILIANO NA WATEJA UKONGA - ILALA

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mkoa wa Kihuduma Ukonga wakiwa katika zoezi la utoaji wa elimu na kufuatilia wateja wenye malimbikizo na madeni ya bili za maji katika maeneo ya Mkoa wa Kihiduma.

Zoezi la ufuatiliaji wa madeni kwa wateja hufanyika nyumba kwa nyumba katika Mikoa yote ya Kihuduma ya DAWASA na huambatana na utoaji wa elimu mbalimbali kuhusu huduma za DAWASA zikiwemo namna ya ulipaji wa bili za maji, ulipaji madeni kwa mikataba pamoja na faida za kulipa bili kwa wakati.

Miongoni mwa faida za ulipaji bili kwa wakati ni kuwezesha mamlaka kufanya maboresho ya huduma, kuendeleza miradi iliyopo na kuanzisha miradi mingine kwa maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma pamoja na upatikanaji wa huduma bora na endelevu kwa wateja.