DAWASA YAKUTANA NA WAKANDARASI WA MIRADI YA MAMLAKA
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imekutana na Wakandarasi (Contractors) na washauri wa miradi (Consultants) inayotekelezwa ndani ya eneo lake la kihuduma na kuwataka kuharakisha utekelezaji wa miradi kwa wakati ili kufikisha asilimia 95 ya upatikanaji huduma kwa wananchi mjiini ifikapo 2025.
Akiongea katika kikao hicho, kaimu Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA, Ndugu Kiula Kingu amesema lengo la kuwaita wakandarasi hao na kuwakumbusha utekelezaji wa miradi ya majisafi na usafi wa mazingira kwa wakati ili kurahisisha upatikanaji wa huduma.
“Tumepewa jukumu la kuhakiksha Wananchi wanapata huduma kwa wakati, nyie ni daraja muhimu katika kuhakikisha huduma ya Maji inawafikia wengi na hii itawezekana kwa usimamizi madhubuti wa miradi itakayokamilika kwa wakati na kuleta tija” alisisitiza Ndugu Kiula
“Ni wito wangu kwenu nyote kuongeza umakini katika kusimamia na kukamilisha miradi hii kwa wakati kwani ni agizo la Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kuona mnakamilisha miradi kwa wakati”. aliongeza Mtendaji MKuu wa DAWASA
Kwa upande wake mwakilishi wa Wakandarasi kutoka Kampuni ya Sinohydro Ltd ambao ni wasimamizi wa Mradi wa bwawa la Kidunda, Ndugu Ma Zlheng ameishukuru DAWASA kwa kikao kazi cha pamoja na kuahidi kusimamia utekelezaji wa miradi kwa wakati ili kutoa tija kwa Wananchi.