DAWASA YAGAWA VIFAA KWA WAKAZI WA MBURAHATI HADI SINZA
19 Mar, 2024
Habari njema kwa wakazi wote wa maeneo ya Mburahati, Tandale, Tabata Dampo, Makanya, Ndugumbi, Mabibo, Manzese, Mzimuni na Sinza, kuwa ofisi za DAWASA Magomeni inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi.
Zoezi hilo linaenda sambamba na utoaji wa elimu ya utunzaji wa miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano na malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.
Takribani wateja 55 wa maeneo hayo wanatarajia kunufaika na huduma ya majisafi.
Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0735 451 862 (DAWASA Magomeni).