DAWASA KUENDELEA KUUNGA MKONO SEKTA YA ELIMU NCHINI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeendelea kuonesha nia ya dhati ya kushirikiana na Serikali katika kukuza sekta ya elimu hususani kwenye eneo lake la Kihuduma.
Hayo yameelezwa na Meneja wa DAWASA Mapinga, Ndugu Abraham Mwanyamaki wakati akizungumza katika Mahafali ya darasa la saba Shule ya Msingi Vikawe alipoalikwa kama mgeni rasmi.
"Nimefarijika kwanza kufahamu shule ya Msingi Vikawe ni Moja ya taasisi tunazozihudumia na wanapata maji kwa saa 24, kitendo kinachochangia ukuaji wa elimu shuleni hapa," ameeleza ndugu Mwanyamaki.
Ameongeza kuwa, pamoja na mafanikio mengi waliyoyapata shule hii, zipo changamoto zinazoikabili shule na Mamlaka inazichukua changamoto hizo nakuona jinsi gani wanaweza kuzitatua.
"Kwakutambua changamoto zinazoikabili shule, Mamlaka ipo tayari kuchangia madawati katika shule hii ili wanafunzi wapate mazingira bora ya kusomea na kuongeza ufaulu," ameeleza ndugu Mwanyamaki.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Vikawe ndugu Jegame Selemani ameishukuru DAWASA katika kuchochea ukuaji wa elimu shuleni hapo na ameomba ushirikiano huu katika kukuza sekta ya elimu uwe endelevu.
"DAWASA wamekua nasi bega kwa bega, pamoja na huduma nzuri ya Majisafi wanayotupatia hapa shuleni, lakini sasa wanaenda kutatua changamoto ya Madawati na kuwafanya wanafunzi kua na Mazingira bora ya kujifunzia," ameeleza Mwalimu Jegame.
Mwanafunzi anayehitimu darasa la saba Maulid Juma ameshukuru kwa DAWASA kukubali kutatua changamoto ya Madawati shuleni hapa na anaimani kubwa yatasaidia sana kwa wanafunzi wanaobakia shuleni