DAWASA YABORESHA MIUNDOMBINU MWEMBEBAMIA - TEMEKE
19 Mar, 2024
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeendelea na kazi ya kuboresha miundombinu ya maji katika mtaa wa Mwembebamia uliopo kata ya Chamazi-Mbagala.
Uboreshaji huo umehusisha ulazaji wa bomba za inchi 2 kwa umbali wa mita 1670 na inchi 2.5 kwa umbali wa mita 600 ambapo lengo ni kunufaisha wakazi takribani 1800 waliopo kwenye kata hiyo.