DAWASA YAANZA MWAKA NA WAKAZI WA BUNYOKWA TABATA
19 Jan, 2024
WANANCHI WA TANDIKA HADI KITUNDA WAANZA KUUNGANISHIWA HUDUMA YA MAJI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia mkoa wa kihuduma DAWASA Temeke inaendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi kwa wateja kutoka maeneo ya Tandika, keko, mtoni, Amani, Sigara, Kiwalani, Kurasini na Kitunda
Aidha kupitia zoezi hilo elimu inaendelea kutokea ya utunzaji wa miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji na njia rasmi za malipo ya huduma za maji pamoja na mawasiliano ya Mamlaka na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.
Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0737-730523 (DAWASA Temeke).