Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA MAPINGA WAENDELEA KUUNGANISHA WATEJA WAPYA
22 Apr, 2024
DAWASA MAPINGA WAENDELEA KUUNGANISHA WATEJA WAPYA

Habari njema kwa wakazi wote wa maeneo ya Kiharaka, Kiembeni, Changuaela, Kerege, Kibosha, Mtambani na Kimele kuwa ofisi ya DAWASA Mapinga inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi.

Pamoja na zoezi hilo, elimu mbalimbali zinatolewa ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano, malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.

Zaidi ya wateja 100  wanatarajia kunufaika na huduma ya majisafi.

Kwa msaada  na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja nambari 0800110064 (Bure) au
0735 202121 (WhatsApp tu) 
0734 359622 (DAWASA Mapinga).