Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAR ES SALAAM YA KUSINI WAHAKIKISHIWA UHAKIKA WA HUDUMA
22 Apr, 2024
DAR ES SALAAM YA KUSINI WAHAKIKISHIWA UHAKIKA WA HUDUMA

Ujenzi wa mradi wa maji wa Bangulo unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)  kwa wakazi wa Dar es salaam ya Kusini umefikia asilimia 20 ukitajwa kuleta ahueni ya huduma kwa Wananchi takribani laki nne na nusu.

Mradi huo unaotekelezwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 40 ikiwa ni miezi minne tangu kuanza utekelezaji wake chini ya kampuni ya SINOHYDRO CONSTRUCTION COMPANY, ambao utiaji saini ulifanyika Novemba 17,2023  na kushuhudiwa na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) 

Akielezea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi, msimamizi wa mradi kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi John Romanus amesema kuwa kazi iliyoanza kufanyika ni pamoja  na ujenzi wa basement ya Tanki litakalo hifadhi  lita milioni 9 sambamba na ulazaji wa bomba la kusambaza maji kwa wananchi lenye ukubwa wa inchi nne ambapo hadi sasa bomba hilo limelazwa kwa umbali wa kilomita 5 kati ya Kilomita …pamoja na maandalizi ya ujenzi wa kituo cha kusukuma maji (booster pump).

"Mpaka sasa ujenzi wa mradi huu umefikia asilimia 20 ambapo tumeshamwaga zege tukisubiri kazi ya kusuka nondo kwa ajili ya kusimamisha tanki. Kazi nyingine zinazoendelea ni pamoja na kulaza bomba la nchi nne kwa ajili ya kusambaza maji kwa wananchi na hadi sasa tumeshalaza bomba kwa kilometa 5 huku tukiamini kwa kasi inavyoendelea mradi huu utakamilika ndani ya wakati uliopangwa," amesema. 

Benard Haule , mkazi wa Kilimani amesema Wananchi wanafurahishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo na kuwa na matumaini makubwa ya kukamilika kwani utasaidia kupunguza changamoto ya Maji katika eneo kubwa la kata yao ya …

Mradi wa maji Bangulo umesanifiwa na kutekelezwa na DAWASA  kwa lengo la kuboresha huduma ya maji kwa wakazi  katika majimbo ya Segerea, Ilala, Kibamba, Ukonga, Ubungo na Temeke na unategemea kukamilika Disemba mwaka huu.