Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
CHANIKA KWA MBIKI WABORESHEWA HUDUMA
24 Apr, 2024
CHANIKA KWA MBIKI WABORESHEWA HUDUMA

Kazi ya kubadilisha miundombinu ya mabomba ya majisafi katika Mtaa wa Kwambiki, Kata ya Chanika imekalishwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa Kihuduma wa Ukonga.

Kazi hiyo imehusisha ubadilishaji wa bomba la inchi 2 na kuweka la inchi 3 kwa umbali wa mita 50 pamoja na ufungaji wa valvu ya inchi 3 kwenye eneo hilo kwa lengo la kuboresha msukumo wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Kwa Mbiki, Kwa Zoo na Chikila.

Maboresho haya yanaenda kutatua changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji kwa wakazi zaidi ya 1200 wa maeneo ya Kwa Mbiki, Kwa Zoo na Kwa Chikila.

DAWASA inaendelea kuwasihi wananchi kutoa taarifa za mara kwa mara endapo watabaini uvujaji katika maeneo yao kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) na mitandao ya kijamii ya mamlaka.