Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
JE WEWE NI MKAZI WA MIVUMONI NA MAENEO JIRANI? 
02 Sep, 2021
JE WEWE NI MKAZI WA MIVUMONI NA MAENEO JIRANI? 

JE WEWE NI MKAZI WA MIVUMONI NA MAENEO JIRANI? 

Habari njema kwa wakazi wa maeneo ya Mivumoni, Muungano, Nyakasangwe, Goba, Salasala, Kilimahewa juu, Kilimahewa, Kinzudi, Madale, Tegeta 'A', Kulangwa, na Kisanga kuwa zoezi la utoaji vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya maji linaendelea katika ofisi za DAWASA Mivumoni. 

Zoezi hili lililohusisha ugawaji wa vifaa vya maunganisho Mapya kwa wateja 100 limeenda  sambamba na utoaji elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, njia rasmi za malipo ya ankara na huduma nyingine za DAWASA. 

Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0734 355755