BONYOKWA NA KISUKURU WAPEWA UHAKIKA WA HUDUMA - ILALA
23 Feb, 2024
Mradi wa kuboresha huduma ya maji Bonyokwa uliofikia asilimia 70 ya utekelezaji wake huku ukihusisha ujenzi wa bomba kubwa na kufunga pampu ya kusukuma maji (Booster pump) unatajwa kwenda kujibu changamoto za kihuduma katika maeneo hayo.
Kukamilika kwa kazi hii kutasaidia kuongeza upatikanaji maji katika maeneo ya Bonyokwa kwa Kichwa, Kwa Dani Mrwanda, Shedafa, Macedonia, mnara wa voda, Chuo cha Masanja, Bonyokwa Kisiwani, JKT B, Msikiti wa Kijani, Mwisho wa Rami, Viwanja vya JKT na baadhi yatanufaika katika kata ya Kisukulu.