BOKO MNEMELA WABOROSHEWA HUDUMA MAJI
06 Sep, 2023
Zoezi la kubadilisha bomba la inchi 8 na kuweka bomba la inchi 12 kwa lengo la kuongeza msukumo wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Boko Mnemela na Mwanalugali waliopo kwenye mji wa Kibaha.
Kazi hii ambayo imetekelezwa na Watumishi wa DAWASA Kibaha inanufaisha wakazi 15,000 wa maeneo tajwa ambao walikuwa wakipata huduma kwa msukumo mdogo.
Mamlaka inaendelea na kazi ya kuboresha huduma ya maji kwa wananchi wote ili kuhakikisha inakamilisha malengo ya Serikali ya kusambaza majisafi kwa wananchi wote.