Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
BAGAMOYO WABORESHA HUDUMA KWA WATEJA, WANANCHI WAISHUKURU DAWASA
03 Jul, 2023
BAGAMOYO WABORESHA HUDUMA KWA WATEJA, WANANCHI WAISHUKURU DAWASA

BAGAMOYO WABORESHA HUDUMA KWA WATEJA, WANANCHI WAISHUKURU DAWASA

Na David Nkulila

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa kihuduma DAWASA Bagamoyo imeendesha zoezi la ubadilishaji na usafishaji wa dira za maji pamoja na kuzinyanyua kwa kuweka magoli Ili kuziweka katika Hali ya usalama na viwango zaidi.

Hatua hii ni jitihada zinazofanywa na Mamlaka katika kuboresha wateja wake huduma ya majisafi katika maeneo yake yote ya kihuduma.

Akiongelea zoezi hilo Mhandisi wa Uedeshaji na matengenezo Mkoa wa kihuduma DAWASA Bagamoyo John Shija dhumuni la kazi hii ni kuzuia upotevu wa maji kwa mteja kutumia maji bila kulipa lakini pia kurahisisha usomaji wa dira hizo.

"Mpaka sasa jumla ya dira za maji 235 zimesafisha na lengo ni kuwafikia zaidi ya wateja 674 katika maeneo ya Kota za Chuo Cha Mbegani, Kota Polisi, Kota Chuo Cha Adem, NHC, Zinga, Kiromo, Bongwa, Majani mapana, pamoja na Yombo na zoezi hili ni endelevu" ameeleza Mhandisi Shija.

Ndugu Mariam Hamisi mkazi wa Kiromo ameeleza kuwa wamelipokea zoezi hilo kwa furaha kwani kwa kiasi kikubwa itasaidia kupunguza malalamiko yanayotolewa na wateja mara kwa mara.

"Zoezi hili ni muhimu sana, kwa upande wetu wateja tunafurahi kwani baadhi ya mita zilikua hazionyeshi kutokana na ukungu, hii ilileta malalamiko kipindi cha usomaji na ulipaji  wa bili za Maji, sasa tunaimani malalamiko yatapungua" ameeleza ndugu Mariam.

Pamoja na hayo zoezi hili linaloendeshwa na Mkoa wa kihuduma DAWASA Bagamoyo Lina lengo la kufanya dira za maji kusomeka kwa usahihi, kuepeusha malalamiko kwa wateja kubambikiwa bili, lakini zaidi kuongeza mauzo ya maji kwa kuhakikisha maji yanayoenda kwa wateja yanapita kwenye mita nayanasomwa kwa usahihi.