Je wajaua njia mbali mbali za kutoa maoni na malalamiko kama wateja?
Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inapokea na kushughulikia malalamiko kuhusu utoaji wa huduma. Mteja anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa kutumia njia zifuatazo:-
i. Kufika Ofisi za Huduma kwa Wateja (DAWASA).
ii. Kuandika barua pepe (e-mail info@dawasa. go.tz) au barua kwa
Afisa Mtendaji Mkuu)
iii. Kupiga simu ya bure yenye nambari 080011006
iv. Kuweka kwenye makundi mbalimbali ya WhatsApp yaliyoanzishwa na ofisi za DAWASA maeneo tofauti tofauti yakiwaunganisha Wateja wanaoishi katika eneo husika. Maoni, malalamiko na mapendekezo yatafuatiliwa na kufanyiwa kazi kwa haraka na kwa mujibu wa viwango vyetu vya huduma. DAWASA inakaribisha mawazo na maoni kutoka kwa wadau ili kuboresha utoaji wa huduma.