Kamati ya NIFC Yakutana TIC
Wakuu wa taasisi zinazotoa huduma mahala pamoja kwa wawekezaji kupitia Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) wamekutana kwa lengo la kuboresha huduma kwa wawekezaji leo tarehe 24 Novemba, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa TIC. Kikao hiki cha Kamati ya Kitaifa ya Ufanikishaji Uwekezaji (NIFC) kinaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu Kazi. Taasisi ambazo zimeshiriki kikao hicho ni NEMC, Uhamiaji, OWM Idara ya kazi, TRA, OSHA, NIDA, NACTE, TBS, TNBC, TMDA na BRELA.

