Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye amani na utulivu wa kisiasa barani Afrika. Tangu uhuru wake mwaka 1961, nchi haijawahi kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe au mzozo wowote mkubwa wa ndani.

Watanzania wanaendelea kuishi kwa amani na fikra za umoja wa kitaifa bila mgawanyiko wa kikabila. Tangu uhuru mwaka 1961 chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere, Tanzania imeshuhudia awamu tano za kuachiana uongozi kupitia chaguzi huru na haki. Tangu 1992, mihula ya Urais imeendelea kuwa miwili tu (kila muhula miaka 5).