24 Mar, 2022
TANZANIA INVESTMENT CENTER PROVIDES INFORMATION ON THE IMPLEMENTATION OF THE ITRACOM FERTILIZER FACTORY - DODOMA
Kituo cha Uwekezaji TIC kimetoa taarifa kuhusu maendeleo mradi wa Kimkakati wa uzalishaji wa Mbolea unatekelezwa na kampuni ya INTRACOM LIMITED kutoka Burundi ambapo ni mwitikio wa Juhudi ya serikali ya Awamu ya sita ya kuwavutia wawekezaji kutoka nchini mbalimbali kuja kuwekeza hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Dkt. Maduhu Kazi amesema Kampuni ya Itracom imesajiliwa TIC kwa lengo la kutekeleza mradi wa sekta ya viwanda wa kuzalisha Mbolea. Mradi huu unatarajiwa kutekelezwa kwa muda wa miaka mitatu kuanzia 2021 hadi 2024 Mradi huu ni moja ya Ushuhuda kuwa mpango Mkakati wa Taifa wa kuhakikisha Agenda ya Tanzania ya Viwanda vya kimkakati ili kutosheleza kuu muhimu kama ya Kilimo inawezekana kwa kushirikiana kwa Sekta binafsi.
Akiongea kuhusu thamani ya mradi Dkt. Kazi alisema Kampuni ya Itracom inatarajia kuwekeza jumla ya Dola za Kimarekani zipatazo Milioni 180 ambazo zitawekezwa katika ujenzi wa kiwanda, ununuzi wa mitambo, na vifaa mbalimbali vinavyohitajika. Mradi huu unatarajiwa kuzalisha tani laki sita (600,000) za mbolea kwa mwaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hii Ndg. Samson …amesema, Itracom itakapokuwa imekamilisha uwekezaji wake, wanatarajia kuwepo kwa jumla ya ajira za moja kwa moja Zaidi ya 3000 za na zisizokuwa za moja kwa moja ni 1500 Mradi huu utakuwa umechangamsha sana eneo hili la viwanda la Nara Mjini Dodoma.
Uanzishwaji wa kiwanda hiki utasaidia kupunguza matumizi yetu ya fedha za kigeni kwa kuagizia bidhaa za Mbolea nje ya nchi. Kwani Kampuni hii itakapofikia miaka Kumi ya Uzalishaji itaokoa fedha za kigeni Zaidi ya dola Bilion 3.5 zinazotumika kuagiza mbolea nje ya nchi alimazia Dkt. Kazi.

