Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Tanzania Investment Centre

TIC logo

News

12 Nov, 2021
KIKAO KAZI CHA FURSA ZA UWEKEZAJI KUTOKANA NA MRADI WA RELI YA KISASA (SGR)
KIKAO KAZI CHA FURSA ZA UWEKEZAJI KUTOKANA NA MRADI WA RELI YA KISASA (SGR)

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu Kazi amefungua kikao kazi cha Kamati Maalum Jijini Dodoma. Kikao hicho muhimu kiliitishwa kwa ajili ya kujadili miradi mbalimbali ya Uwekezaji iliyoibuliwa kutokana na Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR).

Baadhi ya Taasisi zilizoshiriki mkutano huo ni pamoja na Shirika la Reli Tanzania (TRC), Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Fedha na Mipango, Mamlaka ya Ukanda Maalum ya Uwekezaji (EPZA), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Benki ya CRDB, NMB, NBC, TADB na TIB.

Katika kikao hicho Dkt. Kazi ameeleza kuwa tayari TIC kwa kushirikiana na wadau husika, kimeibua miradi 30 na kati ya miradi hiyo 15 imeidhinishwa na ipo tayari kwa ajili ya kunadiwa. Aidha Dkt. Kazi ametumia nafasi hiyo kuiomba sekta binafsi kuwapa taarifa wadau wake wa ndani na nje ya nchi juu ya uwepo wa fursa hizo.

Miradi hiyo 15 ni pamoja na mradi wa mabango katika vituo vya SGR na kwenye mabehewa, uboreshaji wa huduma za utunzaji wa mizigo, mradi wa machimbo ya mawe, na vituo vya habari katika vituo vya SGR.

Aidha Dkt. Kazi amebainisha kwamba, kuna miradi 5 ya kipaumbele kati ya 30 iliyoainishwa ambayo inatakiwa kutekelezwa na Serikali mapema kabla ya miradi mingine kuanza. Miradi hiyo ni ramani za msingi zinazozunguka SGR na maeneo ya karibu, mpango na upimaji ardhi pembezoni mwa SGR na kutenga ardhi kwa ajili ya uwekezaji, usambazaji na ugawaji wa meme, usafirishaji na usambazaji wa gesi asilia na huduma za maji

 

Feedbacks

Feedback, Complaint or Opinion:

TISEZA AI Assistant ×